The House of Favourite Newspapers

Mwingine Auawa kwa Mlipuko Uganda

0

IKIWA ni takribani siku moja tu tangu tukio kama hili litokee, mtu mmoja ameuawa na wengine amba idadi yao haijajulikana wamejeruhiwa leo Jumatatu, Oktoba 25, 2021 kufuatia mlipuko ulioripotiwa kwenye basi lililokuwa likisafiri kwenye barabara ya Kampala-Masaka nchini Uganda.

 

Vyombo vya habari nchini Uganda vimeripoti kuhusu tukio hilo ambapo imeelezwa kuwa maafisa wa vyombo vya usalama walikuwa wamezingira eneo la tukio huko Lungala, Wilaya ya Mpigi kwenye barabara ya Kampala-Masaka ambapo mlipuko ulitokea ambapo mpaka sasa Polisi hawajatoa taarifa kuhusu mlipuko huo.

 

Hapo awali Kikundi cha Islamic state (IS) kilidai kuhusika na shambulio la bomu lililomuua takriban mtu mmoja katika mji mkuu wa Uganda Kampala, juzi Jumamosi usiku. Kikundi hicho cha wanamgambo kiliyasema hayo katika taarifa iliyotangazwa kwenye chombo cha habari chenye uhusiano na kundi hilo jana Jumapili.

 

Kikudi hicho kilisema kwamba baadhi ya wajumbe wake walitekeleza tukio hilo kilabu ambapo “wajumbe na majasusi wa serikali ya Uganda walikuwa wamekusanyika” mjini Kampala.

 

Bomu hilo, lilikuwa limesheheni vyuma vyenye ncha kali, liliulenga mgahawa huo maarufu kwa uuzaji wa nyama ya nguruwe (kiti moto) uliopo katika Mji Mkuu wa Kampala.

 

Taarifa zilizokusanywa zinaonyesha kuwa wanaume watatu, waliojifanya kuwa ni wateja, walitembelea mgahawa huo, wakaweka mfuko wa plastiki chini ya meza na kuuacha muda mfupi baada ya kulipuka.

Leave A Reply