The House of Favourite Newspapers

Mwinjilisti Awashukia Manabii

1

1.Mwinjilisti, Daudi Mashimo (kulia) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).Kulia kwake ni Mtumishi wa kanisa la Carvaly lililopo eneo la Mwenge Dar, Dickson Martin. Mwinjilisti Mashimo (kulia) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani). Kulia kwake ni Mtumishi wa kanisa hilo, Dickson Martin.
2.Mwinjilisti,Daudi  Mashimo (kulia) akionesha moja ya karatasi aliyoindaa yenye ujumbe ambayo alisema atabandika kwenye mabango ya matangazo .Mwinjilisti Mashimo (kulia) akionesha moja ya karatasi aliyoindaa yenye ujumbe ambao alisema atabandika sehemu mbalimbali kwenye mabango ya matangazo.
3.Wanahabri wakifuatilia mkutano huo.Wanahabri wakifuatilia mkutano huo.
4. Bango lake-001Kipeperushi lenye ujumbe wake.

MWINJILISTI wa Kanisa la Calvary lililopo maeneo ya Mwenge jijini Dar es Salaam, Daudi Mashimo ‘Komandoo wa Yesu’ amewajia juu viongozi wa dini waliojipa cheo cha unabii kwa kuwapa siku 14 ili wajitokeze kudhihirisha unabii wao na kudai kuwa wakishindwa wasiendelee kujiita manabii.

Mwinjilisti huyo aliyasema hayo leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar alipokuwa akizungumza na wanahabari na kusema kuwa hapa nchini hakuna manabii wa kweli wa kiroho bali kuna manabii matapeli wa kiroho.

Amesema wote wanaojiita manabii huangalia upepo wa tukio fulani na baadaye kufanya maombi ambapo yanapokuwa yametimia hutumia mwanya huo kujitangaza kuwa wao ndio wamefanikisha kubashiri tukio hilo.

Mashimo alidai kuwa kazi yake kubwa ni kupeleka habari njema kwa jamii ili kutokuingia katika matatizo ya kimwili na hata kuondokana na imani potofu miongoni mwa watu wanaoeneza imani zisizokuwa na mashiko huku akisisitiza kuwa manabii hao huanzisha makanisa kwa ajili kujipatia kipato.

Aidha, alisema kwa imani anayoiamini yeye manabii kazi yao kubwa ni kubashiri matatizo ya kijamii kama machafuko ya kisiasa au majanga mbalimbali na kutoa tahadhari.

“Manabii wetu hawa wanaojitangaza siku hizi kazi yao ni kusubiri dalili fulani za matukio zijioneshe ndipo wajitangaze kuwa wao ndiyo wameoneshwa maono ya tukio hilo,” alisema Komandoo wa Yesu.

PICHA/HABARI: DENIS MTIMA/GPL

1 Comment
  1. Prince'otto says

    hazimtoshi nayeye pia. ameona atangaze jina lake kwa stail hiyo ya kijinga. kama yeye naye ni miongoni mwa watumish wa Mungu, atangaze neno la Mungu atajulikana tu. lkn ajue pia tukishamjua thawabu yake imetimilika tayari.

Leave A Reply