The House of Favourite Newspapers

Mzazi mwenza wa Rose Ndauka anaswa akijipikia futari!

0

Mume wa Rose Ndauka (1) Mzazi mwenzie na staa wa filamu Rose Ndauka, Maliki Bandawe akipika futari.

Imelda Mtema, Amani

Mwanamuziki ambaye ni memba wa Kundi la TNG waliotamba na nyimbo ya Bongo.Com, Maliki Bandawe ambaye pia ni mzazi mwenzie na staa wa filamu Rose Ndauka, hivi karibuni alinaswa jikoni akijipikia futari.

Mume wa Rose Ndauka (2)

Maliki ambaye awali alikuwa akiishi pamoja na staa huyo alinaswa akiwa jikoni ameshapika kila kitu na alikuwa akiaanda kwa ajili ya kula.

Akizungumza na Amani Maliki alisema kuwa mara nyingi anapenda kupika hata wakati anaishi na Rose, hivyo kuingia kwake jikoni yeye siyo ishu kabisa kwa kuwa hakuna chakula ambacho kinampiga chenga kupika.

rose_ndauka776Rose Ndauka na Mwanaye.

“Kupika kwangu siyo ishu na mara nyingi sana napika na ninapenda sana kufanya hivyo hata nilipokuwa naishi na Rose yaani ni kitu ninachokipenda sana.”

mzazi mwenzie na staa wa filamu Rose NdaukaRose Ndauka na Mzazi mwenziye.

Mwanamuzi huyo ambaye alijaliwa kupata mtoto mmoja wa kike na staa huyo waliompa jina la Narvin, walitengana miaka miwili iliyopita  ambapo hawakuwahi kuweka wazi sababu za kuachana kwao kwa sababu kila mmoja alikuwa akimshtumu mwenzake ndiyo chanzo.

Leave A Reply