The House of Favourite Newspapers

Mzazi Mwenza wa Young D Abanwa Kumwacha Mwanaye

0
Mamisa amir, mzazi mwenzake na Young D

BAADA ya kudaiwa kumuacha mwanaye mchanga mwenye umri wa miezi saba kwa bibi yake ambaye ni mama mzazi wa mwanamuziki David Genzi ‘Young D’, mwanamama, Mamisa Amir amebanwa juu ya ishu hiyo na kueleza sababu ya kufanya hivyo.

 

Kwa mujibu wa chanzo makini, kwa sasa mtoto huyo wa kike aitwaye Tamar yupo kwa bibi yake maeneo ya Tabata baada ya Young D kushindwa kuelewana na Mamisa hivyo mama mzazi wa Young D kuamua kumchukua mjukuu wake huyo.

David Genzi ‘Young D’

Akizungumza na Wikienda baada ya kubanwa kuhusu ishu hiyo, Mamisa alikiri Tamar kulelewa na mama wa Young D kufuatia makubaliano yaliyofanyika ambapo mama huyo alisema apewe amlee mjukuu wake.

 

“Mapenzi hakuna tena kati yangu na Young D, ndiyo maana familia yake iliamua kumchukua Tamar ili kumlea kwani nisingeweza kumlea kwa sababu ninafanya kazi. Nikitaka kwenda kumuona ninakwenda kama kawaida na hata nikitaka kulala huko wiki moja, ninalala,” alisema Mamisa.

 

Stori: Gladness Mallya | IJUMAA WIKIENDA| Dar

Juma Nature na Wanaume TMK wafunika Show ya Dar Live

Leave A Reply