MZEE AKILIMALI AMVAA YONDANI

Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali.

 

KATIBU wa Baraza la Wazee wa Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali amemgeukia aliyekuwa nahodha wa timu hiyo, Kelvin Yondani kwa kumtaka abadilike ili aweze kuendana na hali ya timu kwa sasa.

 

Hivi karibuni, kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera raia wa DR Congo alimvua unahodha beki huyo kutokana na madai ya utovu wa nidhamu ikiwemo kuchelewa kuripoti mazoezini baada ya mapumziko mafupi bila ya kuwepo kwa taarifa yoyote huku jukumu hilo akimpa mshambuliaji Ibrahim Ajibu.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Mzee Akilimali alisema kuwa Yondani anapaswa kurekebisha tabia hiyo kutokana na ukubwa wake kwenye timu hiyo.

Kelvin Yondani.

“Ni kweli Yondani kama ni kipenzi changu lakini katika masuala ya timu kocha ndiyo anajua na alichokifanya kwake anaona kipo sahihi siwezi kupinga maana kiongozi anapaswa kuwa mfano kwa wengine.

 

“Kikubwa nadhani anatakiwa ajirekebishe halafu anafahamu yeye ni nani ndani ya Yanga kwa sababu ukiangalia kwa wachezaji wakubwa kwa maana ya muda mrefu amebakia yeye na wachache ambao wanam

fuatia hivyo ni muhimu kuya fanyia kazi hayo,” alisema Mzee Akilimali.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

KARIBU ujiunge na familia ya marafiki wa Global TV Online – Club sasa, uwe wa kwanza kupata video zote za Global TV, video za hamasa kutoka kwa Eric Shigongo, breaking news za matukio yote duniani, michezo na dondoo za afya. Utapata nafasi ya kuingia bure na kutazama shoo, matamasha, semina na burudani zinazoandaliwa na Global TV mikoa yote Tanzania.
Pia, ukiwa na tatizo la kifamilia mfano misiba, kuuguliwa na majanga, marafiki zako wa Global TV Club tutakusaidia.
 
Pia, tutakuunganisha na mtandao wa marafiki zetu waliyofanikiwa ndani na nje ya Tanzania, ili upate mafunzo maalum ya kujikwamua kutoka katika hali duni ya maisha.

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Loading...

Toa comment