The House of Favourite Newspapers

Mzee Majuto Ampa Tano Ngubilu

KOMEDIANI lejendari Bongo, Amri Athuman ‘Mzee Majuto’ amesema kuwa mwaka 2018 ameibuka kivingine baada ya kujikita kwenye sinema za action huku akimpa tano mwigizaji anayecheza naye kwa sasa, Maurus Laurent ‘Ngubilu’.

 

Mzee Majuto aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, sinema iliyoingia sokoni juzikati ya Mjeshi Mtata ndiyo inayomuonesha akifanya vitu vya hatari kwa mara ya kwanza kwenye filamu za action (mapigano).

 

“Nimetaka nioneshe ukali wangu kwenye mambo ya action, lakini ninampongeza kijana wangu Ngubilu ambaye ndiye nimeshirikiana naye, kiukweli yupo vizuri na atafika mbali,” alisema Mzee Majuto akiungwa mkono na Ngubilu.

Stori: Mwandishi Wetu, DarSTORI: Imelda Mtema, Dar, IJUMAA WIKIENDA

LIVE: Sherehe ya Ndoa ya Shilole Usiku Huu Masaki Part – 2

Comments are closed.