The House of Favourite Newspapers

Mzee Mpili Awafungukia Msolla, Injinia Hersi – Video

0

 

Haji Omar ‘Mzee Mpili’ amefunguka kuwa amezungumza na baadhi ya viongozi wa Yanga akiwemo Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msola na Injinia Hersi juu ya mwenendo wa klabu.

 

Mzee Mpili ambaye ni mwanachama wa Klabu ya Yanga kwa siku za hivi karibuni alijivunia umaarufu mkubwa baada ya kumalizika kwa mchezo wa Simba dhidi ya Yanga uliopigwa Julai 3, mwaka huu.

 

Umaarufu huo ulikuja ambapo kabla ya mchezo huo alitamba kuifunga Simba na hatimae jambo hilo likatimia baada ya Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

 

Aliyazungumza hayo kwenye kipindi maalum ambacho kilifanyika jana kwenye ofisi za Global Publishers kupitia kipindi maalum kilichoruka kupitia Global TV na +255 Global Radio.

 

“Nimeanzisha mradi wa kuuza t-shirt kwa ajili ya kuchangia tawi langu la Ikwiriri, nikaamua kutoa t shirt hizi katika kuhakikisha kazi inamalizika kigoma.

“Tawi la Ikwiriri ndio linacheza mpira kutokana na namna ambavyo mimi nimeleta morali kwenye klabu, ushikamano nimeleta na kigoma tunapata matokeo ndani ya uwanja.

 

“Nakaa upande wa wachezaji katika kuchezesha na ninapata nafasi ya kuzungumza na wachezaji kutokana na kutambulika kwani kila mtu ananijua ndani ya Yanga pamoja na Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete.

 

“Niliwaambia wachezaji watulie na kupata nafasi ya kucheza, Simba wanatumia ndani na nje ya uwanja, nasema mpira ni dakika 90 za ndani ya Uwanja ila sisemi natumia njia gani katika kucheza mpira.

 

“Simba walikuwa wanakaa vizuri kwa mshikamano niliwahi kuwaambia Yanga kuwa hawashirikiani na endapo watashirikiana kwa pamoja basi timu itafanya vizuri, mara kila mtu analeta wachezaji wake hii inaleta shida.

SUALA LA MORISSON

“Akili yake waliivuruga na mimi naamini kama angekuwepo Yanga basi angefanya vizuri sana tofauti na sasa, kwa sababu wanasema hayupo kwenye timu ameondoka.

 

“Ndio maana tumepeleka CAS na kesi yake ni nzito na Morisson mwenyewe alitaka kesi yake iamuliwe hapa na mpira wake umeshapotea.

“Tarehe tatu alionyesha kama shoo tu hakufanya chochote kwani tulizuia mpira wake, na kwenye simu yangu sina namba ya Morisson na siwezi kuongea nae.

 

“Mzee Dalali amesema anatangulia kigoma na anaenda kunipiga lakini akumbuke kuwa na Haji Manara alisema hivo hivo kuwa atanipiga tatu kwenye mchezo uliopita na nilimpiga na hela katoa, sahizi sio bao moja itakuwa zaidi ya kuhesabu.

 

“Sisi hatuwezi kubadilisha uwanja ni ule ule pale pale kigoma sisi mipango ya kucheza mpira tumeshamaliza na watu wangu wameshafika.

“TFF wanavuruga mpira kwa sababu Yanga imepeleka makosa nane kwa msimu huu anajua waziri wa michezo lakini hakuna jibu lililorudi mpaka leo, hawasimamii vizuri mpira na walisema wameisahau Yanga.

Simba wana kikosi kizuri lakini mimi na wachezaji wangu wa kuokota okota nitawapiga hivo.

KUMSEMA MSOLA NA HERSI

“Nilimsema Msola kutokana na baadhi ya vitu ambavyo anavifanya na kujichukulia maamuzi, timu inahusika na viongozi, wachezaji benchi la ufundi kuna watu wengine hawana nia nzuri na timu.

 

“Pia suala la Injinia Hersi Said kutangaza juu ya wachezaji ambao wamesajiliwa kwenye timu watu waende kuwapokea uwanja wa ndege hii sio nzuri na yeye amekubali na kusema haitajirudia.

 

SUALA LA HAJI MANARA

“Haji alinifuata na kunipongeza kutokana na kazi ambayo nimeifanya ya kupandisha morali katika timu na kuleta msisimko na amehitaji kunipatia tiketi ya kwenda na kurudi lakini nimemwambia nitampa jibu.

Leen Essau.

 

 

Leave A Reply