The House of Favourite Newspapers

Yanga Yaitungua Ihefu Kibabe 2-0

0

TIMU ya Yanga imefanikiwa kuondoka na alama tatu muhimu kwenye uwanja wa Mkapa baada ya kuifunga Ihefu Fc kwa magoli 2-0, mchezo ulipigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam leo jioni Julai 15.

 

Nyota wa mchezo alikuwa kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’ alipachika magoli mawili yote katika kipindi cha kwanza golila kwanza dakika ya 17’ na dakika ya  37.

 

Yanga wametumia mchezo huo pia kuumuaga mkongwe na mchezaji wa kimataifa wa Rwanda Haruna Niyonzima ambaye ataachana na Wananchi mwishoni mwa msimu huu.

 

Kwa natokeo hayo Yanga inaendelea kusalia katika nafasi ya pili  na alama 73 baada ya kucheza mechi 33 n na kuzidi kuicha Azam Fc yenye Pointi 64, na hata ikishinda mechi zake zlibaki bado hawezi kuishusha Yanga, Azam  ipo Dimbani usiku huu kuvaana dhidi ya Bingwa wa VPL Simba.

Leave A Reply