Mzee Yusuf Afunika Tena Dar Live Akilizindua Jahazi (Picha +Video)

Hadija Yusuf ndiye aliyefungua shoo ya kundi hilo jipya.

Ama kweli Mzee Yusuf ‘Mfalme’ hana mpinzani. Hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya jamaa huyo kufunika ile mbaya kwenye shoo aliyopiga tena usiku wa kuamkia leo ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live ambapo alikuwa akilizindua upya kundi lake la Jahazi Modern Taarab.

Mke wa Mzee Yusuf, Leyla Rashid akifanya yake.

Mzee amepiga shoo hiyo kwa mara ya pili ukumbini hapo baada ya ile ya Narudi Mjini ambayo ikuwa yakwanza tangu arudi kwenye ulimwengu wa taarab.

 

Mishi Zele (kushoto) na Miriam Amour wakiwajibika.

Katika shoo hiyo Mzee alizindua rasmi kundi lake na kulipa jina lilelile la Jahazi.

Mzee Yusuf (katikati) akifanya makamuzi.

Kabla ya kuzindua jina hilo aliwauliza mashabiki kama walikuwa wakipenda alipe jina gani kundi hilo ambapo umati mkubwa uliokuwa ukumbini hapo ulilipuka kwa mayowe na kusema Jahaziii… huku wachache wakisema Safinaaa…

Mashabiki wakijimwaya kwa raha zao.

Msemo wa wahenga usemao Wengi wape ndiyo uliochukua nafasi ingawa hata hivyo jina la Jahazi lilikuwa limeshaandaliwa hivyo kilichofanyika ni kulizindua tu jina hilo.

Mishi Zele akikamua.

Katika kundi hilo Mzee alikuwa na waimbaji wake aliokuwa nao Jahazi la kwanza akiwemo Khadija Yusuf, Leyla Rashid, Miriam Amour, Mishi Zele, Fatma Kassim, Mwasity Mbwana, Ally Jay, Mussa Mipango, Jumanne Ulaya na wengineo.

Mzee Yusuf akimchagiza mpiga solo wake, Jumanne Ulaya a.k.a Mkono wa Biashara.

Wadau walivyolizindua upya kundi la Jahazi Modern Taarab.                                                                                                                                                                                                                                         

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS / GPL

Toa comment