The House of Favourite Newspapers

Mzee Yusufu Kufumbua Fumbo Dar Live

0

BAADA ya Mfalme wa Taarabu hapa nchini, Mzee Yusufu kuja na Narudi Mjini, sasa aja kufumbua fumbo na shoo ya kukata na shoka pale Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar.

 

Akizungumza na Gazeti hili muandaaji wa shoo hiyo Rajab Mteta (KP) amesema, Septemba 25 mwaka huu pale Dar Live Mbagala, Mzee Yusufu atakua na jambo lake, lengo ikiwa ni kutambulisha bendi mpya na wasanii wake, ambayo imekuwa ni fumbo kwa mashabiki.

“Mashabiki wanaombwa kufika kwa wingi, kwani Mzee anatarajia kufanya makubwa. Baada ya shoo ya kukata na shoka ya Narudi Mjini, hii ya sasa itakuwa ni zaidi maana ataenda kutambulisha bendi yake mpya na wasanii atakaofanya nao kazi.

 

“Kiingilio kitakuwa ni shilingi 10, 000 tu na kutakuwa na wasanii kibao ambao watamsindikiza mfalme Mzee Yusufu, hivyo mashabiki wafike kwa wingi kwa ajili ya kupata burudani,’’ alisema KP.Aliongeza kuwa, muda ni kuanzia saa mbili usiku hadi majogoo, hivyo mashabiki wanaombwa kuwahi ili wasikose nafasi maana matarajio ni kuwepo kwa mafuriko ya watu.

Stori: Happyness Masunga | Amani

Leave A Reply