The House of Favourite Newspapers

Mzozo wa Ukraine: Afisa wa China Akutana na Balozi wa Urusi – Live Updates

0

Afisa wa wizara ya mambo ya nje ya China alikutana na balozi wa Urusi nchini China siku ya Alhamisi ili kubadilishana mawazo kuhusu uhusiano wa nchi hizo mbili, kilisema chombo cha habari cha Reuters kikinukuu wizara ya mambo ya nje ya China.

 

Cheng Guoping, Kamishna wa Mambo ya Nje na Masuala ya Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje ya China, alikutana na Andrey Denisov wa Urusi na kubadilishana mawazo kuhusu ushirikiano wa pande hizo mbili dhidi ya ugaidi na usalama, ilisema ripoti hiyo.

 

Mkutano huo unakuja huku kukiwa na hofu kwamba Beijing itakubali ombi la Urusi kutoa msaada wa kijeshi katika uvamizi wake nchini Ukraine.

 

Marekani imeonya kuwa “haitasita kuitoza gharama kubwa ” China ikiwa itaisaidia Urusi moja kwa moja na zana za kijeshi.

 

Leave A Reply