The House of Favourite Newspapers

Mzungu Atamba Kumaliza Cheka Raundi ya Tano

0

BONDIA (2)Kutoka kushoto ni, Juma Msangi (promota wa mpambano huo), Ostaz Yassin Abdallah (Rais wa Chama cha ngumi za kulipwa Tanzani -TPBO), Juma Ndambile (Mkurugenzi wa Kampuni ya Advanced Security), Geard Ajetovic (bondia kutoka serbia) na wa mwisho ni Aksu Sahhaydar (Kocha wa Ajetovic).

BONDIA (3)BONDIA (4)Mkutano ukiendelea.
BONDIA (5)Ostaz Yassin Abdallah akishikana mkono na kocha Aksu Sahhaydar.BONDIA (6)Ostaz Yassin Abdallah, akifafanua jambo.

BONDIA wa kimataifa, Ageard Ajetovic raia wa Serbia amesema kuwa amekuja nchini kufanya kazi mmoja tu ya hukakikisha anamchapa mapema kabisa mpinzani wake Franacis Cheka ‘SMG’ tena ikiwezekana kwenye raundi ya tano.
Cheka na Ajetovic wanatarajia kupanda ulingoni Jumamosi ya wiki hii kwenye Viwanja vya Leaders Club Kinondoni, katika pambabo la kugombania Ubingwa wa Dunia WBF Intercontinetal.

Akuzungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam, Ajetovia ambaye amekuja na kocha wake Aksu Sahhaydar alisema kuwa nafahamu kuwa Cheka ni bondia mzuri lakini atahakikisha anaitumia nafasi hiyo kufumndisha mchezo huo kwa kuwa tayari ameshakuwa mzee ‘babu’.

“Nimewahi kuja kwa sababu ya kutaka kuzoeza mazingira kabla ya siku ya Jumamosi kupanda ulingoni dhidi ya Franci Cheka kwa sababu natambua kama ni bondia mzuri lakini nimekuja kwa kazi ya kuhakikisha namfundisha namna ya kucheza ngumi kutokana na umri wake kuwa ni mkubwa.

“Mapema tu, nitakuwa nishamaliza pambano, nadhani katika raundi ya nne au tano kazi yangu iwe imeshamalizika kwa sababu Chaka siyo mgeni kwangu na nilishampiga nchini Uingereza mwaka 2008 hivyo hakuna kitakachonishinda ila siwezi kusema kama itakuwa ni KO,” alisema Ajetovic.

Lakini kwa upande wa upande wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Advance Security, Juma Ndambile ambaye pia ni meneja wa Cheka alisema kuwa wameamua kuwashirikisha mabondia chipukizi ambao watacheza mapambano ya utangulizi siku hiyo ni Mohammed Bakari vs Cosmas Cheka, raundi (8) Mustapha Dotto vs Mohammed Matumla (8) wakati Mada Maugo atacheza na Baraka Mwakansope badala ya Dulla Mbabe kama ilitangzwa awali huku LuLu Kayage akitarajia kucheza na Mwanne Haji pambano la raundi Sita.

NA IBRAHIM MUSSA NA MUSA MATEJA/GPL

Leave A Reply