The House of Favourite Newspapers

Na Gode wa Yemi Alade: Kina Vanessa mnaandika lakini?

0

YEMI-ALADE1 Yemi Eberechi Alade.

Na Erick Evarist na Mitandao

MUZIKI mzuri huwa hauhitaji promo. Hauhitaji matangazo katika mitandao ya kijamii ili ukubalike. Mtoto mzuri kutoka Nigeria, Yemi Eberechi Alade amedondosha Wimbo wa Na Gode siku chache zilizopita, ndani ya muda mfupi umekuwa gumzo Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Wimbo huo ambao ameufanya kwa kutumia lugha ya Kiswahili, umekuwa ukipigwa sana katika vituo mbalimbali vya redio na televisheni. Umeongozwa kwa kuombwa na mashabiki wengi wa burudani, bila shaka ni wimbo mzuri.

YEMI-ALADE2Yemi ambaye ni msomi mwenye stashahada ya Jografia aliyoipatia Chuo Kikuu cha Lagos, Nigeria, amepata umaarufu mkubwa akiwa angali na umri wa miaka 26 tu hadi sasa. Japo alianza muziki muda mrefu lakini aliweza kujulikana zaidi mwaka 2009 aliposhinda mashindano yaliyofahamika kama  Peak Talent Show.

Yemi aliachia Wimbo wa Fimisile baadaye (mwaka 2012) akatoa Ghen Ghen Love ambazo zote zilimpatia umaarufu lakini habari ya mjini kilikuwa kibao cha Johnny ambacho alikipika prodyuza maarufu nchini Nigeria, Selebobo. Ukampa shoo kibao ikiwemo ile ya Usiku wa Matumaini mwaka 2014 iliyofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Vanessa-Mdee-1.jpgVanessa Mdee

Wakati dunia ikiendelea kumtazama kama mrembo anayekuja kwa kasi kutoka Nigeria na kufanikiwa kukamua jukwaa moja na wasanii wakubwa duniani kama Mary J. Blige, Shina Peters, M.I, Wizkid, Becca, May D, Waje naYemi Sax, Yemi amewashangaza wana Afrika Mashariki kwa ujio wake mpya wa Na Gode.

Ameuimba kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Akimaanisha Asante. Kila kona sasa hivi Bongo utawasikia watu wakiimba; nasema asante, kwani wewe ni Mungu…ukipata, ukikosa, sema asantee…

Sasa hivi nchi nyingi za Afrika ambazo zinakifahamu Kiswahili vizuri, zimeupokea kwa mikono miwili. Umekuwa gumzo kila kona.

Hivyo ukitazama hiyo ndiyo ilikuwa tiketi ya kutoboa kimataifa. Safari yake kimuziki haitofautiani sana na warembo wetu; Vanessa Mdee, Linnah na wengineo. Wanapaswa kuthubutu kufanya vitu vya tofauti na kuushangaza ulimwengu.

Hakuna kinachoshindikana. Kama Yemi amefanikiwa kuliteka soko la Tanzania kwa kuimba Kiswahili, kwa nini kina Vanessa washindwe kuwafanyia maajabu ya nyimbo kali za Kiswahili na zikakubalika Nigeria?

Leave A Reply