The House of Favourite Newspapers

Nabi Aanza na Pacha ya Makambo, Mayele

0

KATIKA kuhakikisha timu inatengeneza muunganiko mzuri na kufunga mabao mengi katika msimu wa 2021/22, Kocha Mkuu wa Yanga, Mtunisia, Nasreddine Nabi, ameanza kwa kuikomalia safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.

 


Safu ya ushambuliaji ya
Yanga katika msimu ujao inatarajiwa kuundwa na Heritier Makambo, Fiston Mayele, Jesus Moloko na Ditram Nchimbi. Yanga hivi sasa ipo Morocco ikijiandaa na msimu mpya ambapo itakaa huko kwa siku kumi kabla ya kurejea Dar es Salaam.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, alisema kocha Nabi ameanza kutengeneza muunganiko katika safu ya ushambuliaji ambayo ni muhimu kwake ili kuhakikisha wanatumia nafasi wanazozipata.

 

Mwakalebela alisema kuwa, kocha huyo juzi Jumanne alianza program yake ya kwanza kwa kuwapa mbinu washambuliaji wake jinsi ya kufunga mabao.Aliongeza kuwa, program hiyo iliendana na fitinesi wanayoifanya mazoezi ya asubuhi kabla ya jioni kufanya ya kimbinu zaidi.

 

“Tangu tumefika timu imekuwa ikifanya program mbalimbali kwa mazoezi ya utimamu wa mwili kwa maana ya fitinesi uwanjani.“Pamoja na mazoezi ya kimbinu jinsi ya kufunga mabao ikiwashirikisha washambuliaji pamoja na viungo katika kucheza mipira ya kona, faulo na krosi.

 

“Hiyo ni kuhakikisha timu inatengenezeka kwa haraka kwa maana ya kucheza kitimu pamoja na kuelewana wachezaji haraka,” alisema Mwakalebela.

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

Leave A Reply