The House of Favourite Newspapers

Nabi: Tuliwazidi Mbeya City Kila Kitu

0

NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga, yenye pointi 36 ikiwa nafasi ya kwanza kwenye ligi kuu, amesema kuwa waliwazidi wapinzani wao Mbeya City walio na pointi 23 kwenye kila kitu ndani ya dakika 90, kasoro kuwafunga tu ndio walishindwa.

Juzi, Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Yanga 0-0 Mbeya City ambapo jitihada za Fiston Mayele mwenye mabao sita na pasi mbili kuweza kumtungua Deogratius Munishi, ziligonga mwamba.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Nabi alisema kuwa walikwenda uwanjani na mbinu tofauti za kusaka ushindi na walikuwa wakibadilika kila wakati lakini hawakupata matokeo.

“Ukizungumzia mchezo ambao tumecheza mbele ya Mbeya City, tuliweza kuwazidi kwenye kila kitu kasoro tulishindwa kuwafunga, hayo ni matokeo na huwezi kuyabadili kwa kuwa yametokea na wachezaji walipambana, wanastahili pongezi.

“Ukianzia nafasi ambazo tulitengeneza zilikuwa ni nyingi, uwezo wa kumwiliki mpira ulikuwa ni mkubwa lakini ambacho nilikiona ni kwamba kipindi cha kwanza tulikuwa tunapoteza mipira mingi hasa kwenye upande wa viungo.

“Hilo lipo na hainqa maana kwamba wachezaji wetu watakuwa bora muda wote, inatokea hivyo, tunakwenda kuyafanyia kazi makosa yetu ili kuweza kurudi tukiwa imara zaidi,” alisema Nabi.

LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam

Leave A Reply