The House of Favourite Newspapers

Nabii atangaza vita na mahawara

0

Nabii wa Kanisa la New Revelation lililopo Buza Kipera jijini Dar, Yaspi Bendera akiwabariki wanandoa hao.

MAKUBWA! Nabii wa Kanisa la New Revelation lililopo Buza Kipera jijini Dar, Yaspi Bendera ametoa kali ya mwaka kwa kusema atapambana na watu wanaoishi bila ndoa ‘mahawara’ ili kuhakikisha wanafunga ndoa.

Nabii huyo aliwafungisha ndoa waumini wake 20 huku akisema alichowataka wao ni kununua shela (gauni la bi harusi) tu ambapo sherehe ilifanyika kanisani hapo mpaka saa tatu usiku.

Wakati wa kufungisha ndoa hizo, nabii huyo aliwauliza wanandoa kwa pamoja na wao wakawa wanajibu kwa pamoja tofauti na zile ndoa za kumuuliza kila mwanandoa.

…Wakiwa kwenye picha ya pamoja.

Akizungumza na gazeti hili nje ya kanisa lake baada ya kufungisha ndoa hizo za kihistoria, Nabii Yaspi alisema taifa linakosa maadili kutokana na uwepo wa vitendo vya uzinzi vilivyohalalishwa na watu kupitia uchumba sugu.

Akifafanua hapo, nabii huyo alisema ni jambo la viongozi wote, hasa wa dini na serikali kupinga vikali vitendo hivyo na kusema yeye kupitia kanisa lake atapita nyumba kwa nyumba kuwafungisha ndoa watu.

“Taifa linakosa maadili kwa sababu ya mambo yanayohalalishwa lakini hayatakiwi. Nimeoneshwa na roho wa Mungu kuwa natakiwa kupita nyumba kwa nyumba kuwafungisha ndoa wachumba sugu na hakuna atakayepinga kwa uwezo niliopewa,” alisema Nabii Yaspi.

Leave A Reply