The House of Favourite Newspapers

Naibu Waziri ‘Ahamia’ Rasmi Shamba – Pichaz

NAIBU Waziri wa wa Kilimo, Omary Mgumba,  amewahamasisha wakulima wote nchini kuzitumia vizuri mvua zinazoendelea kunyesha kwa kupanda mazao mbalimbali yakiwemo ya  vyakula na matunda kama sehemu ya kuhakikisha kunakuwa na usalama wa chakula na lishe nchini.

Ametoa hamasa hiyo jana Novemba 24, 2019 akiwa katika moja ya mashamba yake Kitongojini Misala Mkuyuni Morogoro (V) alipokuwa akiwajibika kupanda miembe na mihogo katika kipindi hiki cha mvua za vuli.

Ametumia nafasi hiyo kueleza umuhimu wa kila mkulima kuhakikisha anatumia msimu wa mvua za kilimo vizuri na kuwashauri wakulima waandae mazao mchanganyiko ili kuhakikisha kunakuwa na chakula cha kutosha na cha uhakika nchini.

Pia amemaliza ziara yake ya siku saba ya kuhamasisha wananchi jimboni kwake na  mkoani humo kwa kuzitumia mvua vizuri na ameshiriki kikamilifu kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa ambao umefanyika nchini kote jana Novemba 24.

“Nimekuwa katika ziara kwa siku saba, nimekuja kuhamasisha wakulima kujikita katika kilimo na kutumia mvua hizi vizuri. Binafsi  baada ya kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa, nimeamua kuingia shambani kufanya shughuli za kilimo,”amesema.

Comments are closed.