The House of Favourite Newspapers

Naibu Waziri Ulega Awaongoza Mastaa Mazishi ya Cpwaa (Picha +Video)

0
Mmoja wa waombolezaji akilia kwa uchungu.

NAIBU Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Abdallah Ulega leo aliwaongoza waombolezaji wakiwemo mastaa wa muziki nchini walijitokeza kwenye msiba wa aliyekuwa mwanamuziki mwenzao, Cpwaa aliyefariki jana kwa nimonia.

Alikiba alivyoingia msibani.

Akizungumza msibani hapo Waziri Ulega amesema amefika msibani hapo kama Waziri husika na pia amefika kama rafiki wa marehemu ambaye walifahamiana tangu mwaka 2002 yeye alipokuwa akisoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kilichopo Mlimani na marehemu akiwa anasoma Chuo cha IFM kilichopo Posta, Dar.

Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu Cpwaa.

Waziri Ulega amesema tangu kipindi hicho baada ya kufahamiana na kuendelea alikuwa shabiki mkubwa wa kazi zake za muziki.

Naibu Waziri Ulega (wapili kulia) na waombolezaji wengine wakijiandaa kuuswalia mwili wa marehemu.

“Mimi nimekuja hapa kwa kofia mbili, kwanza nimekuja kama Waziri husika na pili nimekuja kumzika kijana mwenzangu ambaye tulifahamiana kwa muda mrefu tangu mwaka 2002 nikiwa nasoma pale Chuo Kikuu cha Mlimani (UDSM) naye akisoma pale IFM.

Baba yake Cpwaa, Halifa Juma (mwenye miwani) akizungumza msibani hapo.

“Hivyo msiba huu umenigusa kwa namna tofauti hivyo nimeona sina budi kuacha kila kitu na kuhudhuria msiba huu pia naomba kuchukua nafasi hii kuwapa pole ndugu na jamaa wote waliofikwa na msiba huu”. Alisema Waziri Ulega.

Naibu Waziri Ulega (kulia) akizungumza msibani hapo.

Msiba huo ulihudhuria na umati mkubwa wa waombolezaji wengine wao wakiwa wanamuziki wa Bongo Fleva ambapo miongoni mwao ni pamoja na Ali Kiba, Suma Lee, Fid Q, AY, Q Chilla, Beka Fleva, Juma Nature, Temba, Doro wa TMK, Chegge, Inspector Haroun, Madee na wengineo.

AY (kulia) akizungumza na wasanii wenzake msibani hapo kushoto ni Fid Q na anayemfuatia ni Madee.

Mwili wa marehemu uliswaliwa baada nyumbani hapo ulienda kuzikwa kwenye Makaburi ya Mwinyimkuu yaliyopo Magomeni Mapipa, Dar.

HABARI/PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPL

Leave A Reply