The House of Favourite Newspapers

Naibu Waziri Ulega “Tumedhamiria Kuinua Biashara Ya Dagaa Kigoma”-Video

0

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema Serikali ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imejipanga kuhakikisha Dagaa wa Kigoma wanakuwa ni zao la kimkakati kibiashara litakalokwenda kuvutia uwekezaji na kusisimua uchumi wa mtu mmoja mmoja na nchi kwa ujumla.

 

Ulega aliyasema hayo wakati akiongea na Wadau wa Uvuvi alipofanya kikao nao katika Mwalo wa Katonga uliopo Mkoani Kigoma.

 

Alisema kuwa serikali imejipanga kufanya zao la dagaa wa Kigoma kuwa la kimkakati kwa sababu biashara ya dagaa inahusisha watu wengi katika jamii, hivyo kuiimarisha biashara hiyo ni kuwaimarisha wananchi kiuchumi.

Leave A Reply