The House of Favourite Newspapers

Naibu Waziri Utalii Awataka Watafiti Kuibua Vivutio Vipya

0

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii,Mary Masanja amewataka watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam(UDSM) kuhakikisha wanafanya utafiti na kugundua vivutio vya utalii vilivopo katika mikoa ya Kanda ya ziwa.

 

 

Ameyasema hayo leo mapema wakati wa ufunguzi wa Warsha ya utalii endelevu kanda ya ziwa iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha utalii mkoani Mwanza.

‘’Watafiti wanatakiwa kufanya utafiti wa kuainisha bidhaa za utalii katika mikoa yote sita ya kanda ya ziwa’’ Alisema Masanja.

 

 

Amesema Serikali inatarajia kuendeleza na kuvitangaza vivutio vya utalii kanda ya ziwa pia Serikali imeyapandisha hadhi baadhi ya Mapori ya Akiba kuwa na hadhi ya Hifadhi za Taifa, na hivyo kufanya Hifadhi zetu za Taifa kuongezeka na kufikia idadi ya 22 mwaka 2020 toka idadi ya Hifadhi za Taifa 16 zilizokuwepo mwaka 2015.

 

Kwani mpaka sasa katika kanda ya ziwa, Serikali imefanikiwa kuanzisha Hifadhi za Taifa mpya sita ambazo ni Burigi-Chato, Ibanda Kyerwa, Mto Ugala, Kigosi, Nyerere na Rumanyika-Karagwe, hivyo kufanya mtandao wa Utalii katika Kanda ya Ziwa sasa kuwa na jumla ya Hifadhi za Taifa nane (8) ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo, Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

 

 

Aidha kwa upande wake Mratibu wa mradi wa SIDA kutoka Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam(UDSM),Profesa Wineaster Anderson alisema kupitia mradi wa utafiti katika utalii endelevu watafanya tafiti katika kuibua bidhaa za utalii katika mikoa ya Simiyu,Mara na Shinyanga. Alisema kupitia mradi huo, wameweza kufadhili wahitimu nane katika masomo ya PHD.

Na Leah Marco, Mwanza

Leave A Reply