The House of Favourite Newspapers

Naibu Waziri wa Kilimo Ampigia Saluti Mrisho Mpoto

0
William Ole Nasha akimsifia Mrisho Mpoto viwanjani hapo.

 

Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi ambaye ndiye mbunge wa Ngorongoro, William Ole Nasha leo alipotembelea banda la Balozi wa Hifadhi ya Wanyama ya Ngorongoro amempigia saluti mhamasishaji na balozi wa hifadhi hiyo ambaye pia ni Msanii wa nyimbo za asili, Mrisho Mpoto kwa kazi nzuri ambavyo anaifanya ya  kuhamasisha wananchi na wadau wengine kutembelea hifadhi hiyo ili kujionea utalii Wa ndani.

 

Mrisho Mpoto akizungumza na watoto kuhusu vivutio vya utalii vya hapa nchini.

 

Aidha Waziri huyo alisikia baadhi ya maswali yaliyokuwa yakiulizwa na balozi kwa watoto waliofika kwenye banda la Mpoto kuhusu wanyama na vivutio vingine ambao waliyajibu kwa ufasaha na kiwapatia zawadi ya shilingi elfu hamsini vijana watatu wawili wakipata elfu ishirini.

 

 

William Ole Nasha amesema Mpoto ni mfano mzuri wa kuigwa na wasanii pamoja na Watanzania wengine kwa kupenda na kutangaza kilicho chao ili kuvutia watalii kuja hapa nchini kujionea mambo mbalimbali yanayohusu vivutio vya utalii pamoja na wanayama ambao wengine wanapatikana Tanzania pekee kote duniani.

PICHA ZOTE: NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS

Leave A Reply