The House of Favourite Newspapers

Naibu Waziri wa Nishati Aipa Saa Mbili Tanesco Kurudisha Umeme

0

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga Judith Kapinga amelipa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) saa mbili kurudisha uzalishaji wa umeme kwenye kituo cha kuzalisha umeme cha Ubungo I ambacho kimezimika umeme kuanzia usiku mpaka sasa hivi na mitambo sita inayotakiwa kuzalisha umeme kwa sasa hivi haizalishi na hivyo kupelekea baadhi ya Wananchi kukosa umeme.
Kapinga amesema hayo leo September 29,2023 alipotembelea Makao Makuu ya TANESCO, Ubungo Jijini Dar es salaam “Tumefika hapa na leo kwa bahati mbaya pia kituo cha Ubungo I kimezimika umeme kuanzia usiku mpaka sasa hivi na mitambo sita inayotakiwa kuzalisha umeme kwa sasa hivi haizalishi lakini Wataalamu wako saiti wanahakikisha inawaka”
“Nimewaelekeza TANESCO kuhakikisha ndani ya masaa mawili kituo kile kinarudi katika uzalishaji na kama hakitorudi kwenye uzalishaji watafute njia mbadala ya kuhakikisha ndani ya masaa sita yajayo kituo hiki kinarudi kwenye uzalishaji ili hali ya upatikanaji umeme iweze kuimarika”
“Mashine zile sita zinazalisha kati ya megawati 42 hadi 43 lakini kwasababu zimepata hitilafu hizo megawati ziko nje, nimewaagiza warudishe kituo kwenye uzalishaji na umeme upatikane kwa Wananchi”
Leave A Reply