The House of Favourite Newspapers

Nandy: Achomoa Madai Ya Kunasa Mimba!

0

MSANII wa Bongo Fleva, Faustina Charles ‘Nandy’ amesema kuwa watu wengi wana hofu nayo kwamba huenda ni mjazito lakini ukweli ni kwamba hana mimba.

 

Akizungumza na Risasi Vibes, Nandy alisema kuwa, ameshapata maswali mengi kuhusiana na tumbo lake pia kaweka picha ya mwanamke mjamzito kwenye profile yake ya mtandao wa WhatsApp hivyo amekuwa akipokea maswali mengi kuhusiana na hilo.

 

“Kwa kweli sina mimba kuna wakati mwingine watu wananiangalia vibaya yaani wanafananisha shibe na mimba hapo ndipo wanapofeli kabisa,” alisema Nandy ambaye pia inadaiwa penzi lake na msanii wa Bongo Fleva, William Lyimo ‘Billnass’ limevunjika.

STORI NA IMELDA MTEMA | GPL

Leave A Reply