The House of Favourite Newspapers

Nandy Achukua Likizo Ya Muziki

0

KAMA wewe ni mtalii kwenye mitandao ya kijamii, pasi na shaka utakuwa umekutana na jina la Nandy ambaye ni supastaa na Malkia wa Bongo Fleva.

 

Nandy amedumu kwenye muziki na kufanya vizuri kwa miaka kadhaa kutokana na kufanya kazi kwa bidii hivyo ni mmoja wa mastaa wenye utajiri mkubwa Bongo kutokana na mauzo makubwa ya muziki wake.

 

Mrembo huyo amekuwa mfano wa kuigwa na mabinti wengi wanaotamani kuwa kama yeye kutokana na aina ya maisha anayoishi ya kifahari hivyo kila anachofanya au kukisema kinakuwa na matokeo kwa mamilioni ya wafuasi wake.

 

Nandy ambaye kwa sasa amechumbiwa rasmi na rapa Billnass au Nenga ametoa tamko la kushtua wengi akidai kwamba anakwenda likizo ya muziki. Amesema;

 

“Tupate break kidogo…” Kauli yake hiyo inatafsiriwa tofautitofauti; wengine wanasema anataka kusimama kufanya muziki kama alivyofanya Vanessa Mdee ili ajihusishe zaidi na maandalizi ya ndoa yake na Nenga inayotarajiwa kufungwa Juni 25, mwaka huu.

Leave A Reply