The House of Favourite Newspapers

Nangasu Warema Aandaa Kongamano La Kushehereka Siku Ya Utalii Duniani

0

Mkurugenzi wa WiTT Women in Tourism Tanzania Nangasu Warema.

Dar es Salaam, 11 Agosti 2023: Mkurugenzi wa WiTT Women in Tourism Tanzania Nangasu Warema ameandaa kongamano la kusherehekea Siku ya Utalii Duniani kuelekea kilele cha siku hiyo duniani.

Akizungumza na Global Publishers, Nangasu amesema kongamano hilo linalotarajiwa kuwakutanisha wadau mbalimbali wa masuala ya utalii litafanyika katika Hotel ya Peacock jijini Dar.

Nangasu ameendelea kusema kuwa kongamano hilo linatarajiwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu hotelini hapo ambapo kutakuwa na burudani mbalimbali zitakazohusisha utalii na utamaduni wetu.

“Nawaomba wananchi wote na wadau mbalimbali tujitokeze kwa wingi kwenye kongamano hilo.

“Kwa yeyote anayetaka kujua zaidi kuhusiana na kongamano hilo tafadhali angalia namba zetu za mawasiliano kwenye tangazo letu lifuatalo.

“Njoo tufurahi pamoja kwenye kwenye kongamano hilo linalotarajiwa kuwa la aina yake”. Alimaliza kusema Nangasu.

Leave A Reply