The House of Favourite Newspapers

Nape: Nilaumuni kwa ‘Bao la Mkono’

MBUNGE wa Mtama na aliyewahi kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye,  ameshindwa kujizuia na kujikutaka akijibu hoja mbalimbali mitandaoni kufuatia hatua ya mtandao wa JamiiForums kusitisha kutoa huduma tangu jana kutokana na kanuni za maudhui ya kimtandao za mwaka 2018.

Nape amekuwa akieleza hisia zake kuhusu jambo hilo kwa kuandika kwenye mtandao wa Twitter; “Hili la JF linafikirisha! Ukizuia watu kusema wayawazayo unaweza Kutana nao….. kimya kimya!”

 

Idadi kubwa ya wachangiaji walionekana kumnyooshea vidole kutokana na kwamba wakati akiwa waziri wa habari, alipeleka muswada bungeni na sheria ya huduma za vyombo vya habari kwa mwaka 2016 na  vikapitishwa.  Hata hivyo,  Nape aliwataka wachangiaji kutofautisha vitu hivyo kwani ni sheria mbili tofauti.

 

“Nimeuliza hili swali toka mwanzo, kuna uhusiano gani wa hizi sheria mbili? Au tunakaririshwa au hatujui tunachotaka kusema,” alijibu Nape.

 

Wakati wa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015, Nape Nnauye akiwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), alitoa kauli kuwa chama hicho kingeshinda uchaguzi huo hata kwa bao la mkono,  kauli ambayo iliibua mjadala mpana wakati huo.

 

Alichokijibu leo hiki hapa.

Comments are closed.