The House of Favourite Newspapers

Nape Nnauye Awasilisha Hotuba ya Makadirio na Matumizi ya Wizara Bungeni -Video

0

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye akiwasilisha Hotuba ya Makadirio na Matumizi ya Wizara hiyo Bungeni Jijini Dodoma leo tarehe 20 Mei 2022.

 

“Nachukua fursa hii kumpongeza Rais Samia kwa uongozi wake madhubuti katika kipindi hiki cha zaidi ya mwaka mmoja ambacho kimekuwa na maendeleo na uwekezaji mkubwa katika sekta zote zinazogusa Maendeleo ya watu nchini”

 

“Kulingana na Kitabu cha Hali ya Uchumi wa Taifa cha mwaka 2020, Sekta ya Habari na Mawasiliano imekua kwa kasi ya 8.4%. Ukuaji huu unathibitishwa na ongezeko la upatikanaji na matumizi ya huduma za mawasiliano na kusambaa kwa huduma zitolewazo na vyombo vya habari.”

 

“Aidha, Watumiaji wa intaneti wameongezeka kutoka Milioni 29.1 mwezi Aprili, 2021 hadi kufikia Milioni 29.9 mwezi Aprili, 2022 sawa na ongezeko la asilimia 2.7”

 

“Kwa hakika katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wake kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ameonyesha Uzalendo, Uwezo, Ujasiri, Uhodari na Mapenzi yake makubwa kwa nchi yetu na wananchi wake.

 

Kwa hakika katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wake kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ameonyesha Uzalendo, Uwezo, Ujasiri, Uhodari na Mapenzi yake makubwa kwa nchi yetu na wananchi wake”

 

“Katika uchumi wa kidigitali, Sekta zote hufanya kazi kwa pamoja, kwa ushirikiano na muingiliano zikiwezeshwa na mazingira bora ya kidigitili. Mapinduzi haya yanawezeshwa na misingi muhimu ikiwemo Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na Mifumo ya Mawasiliano”

 

“Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa watoa huduma/wawekezaji kujenga miundombinu ya Mawasiliano ya Intanenti ya kasi ili kuongeza wigo wa mitandao na kuimarisha ubora wa huduma za mawasiliano ili kufikisha kasi kwa 80% ya Watanzania ifikapo mwaka 2025.”

 

‘Serikali kupitia TCRA ipo tayari kutoa Masafa kwa watoa huduma ambao wangependa kufanya majaribio ya teknolojia ya 5G. Utaratibu wa kugawa masafa yaliyobainishwa kutumika kwa teknolojia ya 5G utakuwa wa ushindani (Transparent & Competitive Process)”

 

“Hadi kufikia Aprili 30, 2022, Wizara imekusanya jumla ya Shilingi 41,098,538,762.15 kutokana na mauzo ya huduma za Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ambayo ni sawa na 82.2% ya makadirio ya makusanyo ya Shilingi bilioni 50”

“Hadi kufikia tarehe 30 Aprili, 2022 Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (Fungu 68) imepokea jumla ya Shilingi 129,713,798,179.86 kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ambayo ni asilimia 53.7 ya fedha zilizotengwa”

“Hadi Aprili 30, 2022,Wizara imepokea na kutumia Shilingi 6,947,838,745.79 sawa na 84% ya fedha zilizotengwa. Kati ya fedha za matumizi ya kawaida zilizopokelewa Shilingi 2,288,345,600.00 ni za Mishahara na Shilingi 4,659,493,145.79 ni Matumizi Mengineyo”

 

“Katika kuimarisha uhuru wa Vyombo vya Habari, Serikali imetoa jumla ya leseni mpya 19 kwa magazeti hivyo kufanya Jumla ya vyombo vya Habari vilivyosajiliwa kufikia 285” amesema Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye.

⚫️ SIKILIZA + 255 GLOBAL RADIO LIVE: http://ndstream.net/globalradio/ ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave A Reply