The House of Favourite Newspapers

Nasreddine Nabi Ambadilishia Majukumu Makambo

0

KUELEKEA mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar, Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amembadilishia majukumu mshambuliaji wa kikosi hicho, Heritier Makambo ambaye kwa sasa atacheza kama winga ila atakuwa anaingia katikati kusaidiana na Fiston Mayele na Feisal Salum.

 

Yanga wanatarajia kucheza mchezo huo wa ligi dhidi ya Kagera leo kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera, huku kocha msaidizi wa kikosi hicho, Cedric Kaze akitarajiwa kuwepo kwenye benchi la ufundi la timu hiyo.

 

Kikosi hicho kiliwasili mkoani Kagera juzi Jumatatu kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo ambao utapigwa leo Jumatano kwenye Dimba la Kaitaba.

 

Kwa mujibu wa taarifa kutoka chanzo cha ndani cha Yanga, kutoka mkoani Kagera kimeliambia Championi Jumatano kuwa: “Tayari Kaze kwa kushirikiana na Nabi wamebadilisha mfumo kuelekea mchezo wa kesho (leo) Jumatano dhidi ya Kagera Sugar.

 

“Nikuambie kuwa baada ya Kaze kuanza kazi tayari wameanza kufanya baadhi ya mabadiliko kwenye kikosi kuelekea mchezo wa kesho (leo) baada ya kushtukia mipango ya Kocha wa Kagera, Francis Baraza.

 

“Kaze alipoangalia aina ya wachezaji waliopo kwenye kikosi alimshauri Nabi kumuanzisha Makambo kama winga wa pembeni na katikati kumchezesha mshambuliaji Fiston Mayele akishirikiana na Feisal Salum.

 

“Mfumo huo utamfanya Makambo kuwa huru zaidi na kumfanya kuingia katikati akitokea pembeni akiwasaidia Mayele na Feisal ili kuwepo na idadi ya washambuliaji wengi kwenye eneo la mbele,” kilisema chanzo hicho.

 

Leave A Reply