The House of Favourite Newspapers

Nature, JB wa Mabaga Fresh Wapiga Bonge la Shoo Eid, Dar Live

0
Nature (kushoto) na JB wa Mabaga Fresh wakikamua jukwaani.

MBISHI wa Bongo Fleva anayekimbiza tangu muziki huo unaanza mpaka leo Juma Kassim ‘Nature’ na JB wa kundi la Mabaga Fresh, usiku wa leo walipiga bonge la shoo ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar.

JB akiwaimbisha mashabiki.

Kama kawaida Nature bado ameendelea kuwa kipenzi cha wengi kutokana na ngoma zake ambazo hazifi zikiendelea kupendwa na vizazi vinavyochipukia akiwa na JB walipiga bonge la shoo na kuufanya Uwanja wa Taifa wa Dar Live ‘utimkeutimke’ kiburudani kwa jinsi mashabiki waliofurika walivyokuwa wakicheza mapanga shaaa…

Nature akiwapa ‘mswaki’ mashabiki.

JB naye kama kawaida mzee wa porojo za mashairi alitumia muda flani kuwanogesha mashabiki kwa kurap maneno yake ya kuchagiza kwa staili ya akapera (bila biti) na kuwafanya mashabiki waliofurika walipuke kwa mayowe ya kumshangilia.

Mashabiki wakiwa ‘full mzuks’.

Shoo ilihitimishwa na mwanadada Zuchu kutoka Kundi la WCB ambaye alipiga shoo iliyoacha gumzo kwa jinsi naye valivyowanogesha mashabiki waliofurika kwenye kiwanja hicho cha burudani.                                                                                                                                          HABARI NA PICHA ZOTE : RICHARD BUKOS /GPL 

Leave A Reply