The House of Favourite Newspapers

Baada ya Kufungiwa, Asukile Afunguka

0

 

NAHODHA wa kikosi cha Tanzania Prisons, Benjamin Asukile amefunguka kuwa hana pingamizi na maamuzi ya kamati ya mashindano ya kufungiwa michezo mitano na faini ya Shilingi 500,000 kufuatia kukutwa na hatia ya kutoa shutuma dhidi ya Yanga.

 

Jumanne wiki hii Kamati ya Mashindano ya TFF ilimpa adhabu ya kumfungia Asukile michezo mitano na faini hiyo kwa kukutwa na hatia ya kutoa kauli za udhalilishaji dhidi ya Yanga, wachezaji wa kimataifa wa Yanga, shirikisho na mwamuzi.

 

Asukile alitoa kauli hizo mara baada ya mchezo wa Hatua ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho ambapo Yanga walishinda bao 1-0.

 

Beki huyo kaliambia gazeti hili kuwa: “Nimepata taarifa za adhabu yangu kutoka kamati ya mashindano ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), na wala sina pingamizi na maamuzi yao.

 

“Kikubwa ninachoweza kusema ni kuwa bado nasisitiza hizi sheria na kanuni za soka ni kwa ajili ya timu zote, hivyo zizingatiwe kwa ukamilifu kwa kuwa kunapotokea mapungufu ndivyo sintofahamu hutokea.”

Stori: Joel Thomas,Dar es Salaam

Leave A Reply