Asipofunga Zipu…Nay kufa kwa ngoma

NAY (2) Staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Eribaliki ‘Nay wa Mitego’  akijiachia na mrembo mpya mwenye umbo dogo kwenye bwawa la kuogelea katika Hoteli ya White Sands iliyopo Mbezi Beach jijini Dar.

Musa Mateja
KIWEMBE! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Eribaliki ‘Nay wa Mitego’ kunaswa akiwa na mrembo mpya mwenye umbo dogo yaani (mbichii) huku rekodi ikionesha ndani ya muda mfupi ameshabadilisha warembo takriban wanne hali ambayo imesababisha wadau kumpa tahadhari kwamba asipofunga zipu, ataukwaa Ukimwi a.k.a Ngoma, Risasi Jumamosi lina mchongo kamili.

NAY (3)…Akiwa kambeba ndani ya bwawa la kuogelea. 

TUKIO JIPYA
Achana na Siwema Edson, Shamsa Ford, Stella Tilya ‘Chaga Baby’ aliowapitia katika kipindi kifupi, mapema wiki hii Nay amenaswa na mrembo mbichii aliyefahamika kwa jina la Ana wakifanya yao kwenye bwawa la kuogelea katika Hoteli ya White Sands iliyopo Mbezi Beach jijini Dar.

NAY (4)Nay wa Mitego akifanya yake.

ENEO LA TUKIO
Awali, Mbongo Fleva huyo alionekana akiwa ameketi pembezoni mwa Bahari ya Hindi na baada ya saa moja mbele alielekea kwenye bwawa na kuanza kuongelea akiwa ameambana na mrembo huyo.

NEY-1Siwema akiwa na Nay enzi wakiwa wapenzi.

“Amefika (Nay) na vijana kama wanne hivi na huyo mrembo alikuwa wa tano, mwanzo wakati wakija yule mrembo alikuwa karibu na jamaa mmoja bonge sijui ndiye meneja wake wa sasa, kwa hiyo muda wote nilihisi huyo demu ni wa Bonge kumbe ilikuwa zuga tu maana baada ya kuanza kuogelea demu akaonesha wazi kuwa ni mali ya Nay kwani alikuwa anamfanyia kila linalostahili mtu na mpenzi wake kufanyiana,

AONYWA KUHUSU NGOMA
“Halafu huyu jamaa atakufa kwa ngoma asipokuwa makini maana anabadili warembo kama kitu gani.

Msururu wake unamweka pabaya. Kuna warembo wengi sana kawapitia, maarufu na wasio maarufu. Juzikati alikuwa na Siwema, mara Shamsa, ghafla nikasikia yupo na Chaga Baby leo tena ana kifaa kipya, asipofunga zipu ngoma inamuiita,” alinyetisha mdaku mmoja aliyeshuhudia tukio hilo.

Chaga Baby akiwa katika pozi.

‘KANGAA FOTO’
Kama vile staa wa dansi kutoka Kongo, Koffi Olomide anavyoimba katika wimbo wake wa Selfie, ndivyo paparazi wetu alivyoanza kumtandika picha za kutosha Nay na mrembo huyo walipokuwa wakioga kwa kushikana shikana maeneo ‘muhimu’ ambapo wote kwa pamoja walionekana kufurahi.

WALA PIZZA
Kama hiyo haitoshi, wawili hao baada ya kujiachia katika bwawa hilo kwa zaidi ya saa mbili, walitoka na kuagiza msosi unaojulikana kwa jina la ‘pizza’ ambapo pia walikula kwa staili ya mtu na bebi wake bila kuhofia macho ya watu.

IMG_0093Nay wa Mitego akiwa na Shamsa Ford.

NAY ABANWA, ACHEKA
Baada ya paparazi wetu kukusanya ushahidi wa kutosha juu ya matukio yake ya kimahaba ndani ya maji, alimbana Nay ambaye alishindwa kutoa majibu yaliyonyooka kama kweli aliyekuwa naye ni kifaa chake kipya ama laa!

“Dah, wewe umefikaje hapa na umenionaje? Au kuna mtu kakulengesha nini kwangu, maana si rahisi mwandishi kama wewe kuja hivihivi tu hapa! Si bure utakuwa umepewa umbeya huu na mtu.

ney_wa_mitego_nishaNisha akiwa na Nay.

Risasi Jumamosi: Sasa huyu ndiye mpya au unawachanganya pamoja na yule wa Marekani, Chaga Baby?

Nay: Ebwana huyu anaitwa Ana ni mtu wangu tu, nipo na masela zangu wengine, tumekuja kuogelea kwa raha zetu so haya ni maisha fulani ambayo kila mtu anatakiwa kuwa nayo na kujiachia kwani kuna tatizo?

Risasi Jumamosi: Hauogopi Ukimwi kujiachia na warembo tofauti?
Nay: Kwani nimekwambia huyu ni mtu wangu? Mimi niko makini kweli na suala la ngoma. Naomba uniache niondoke naona unaniharibia siku.

MSURURU WA NAY
Ukiondoa Siwema, Shamsa, Chaga Baby huko nyuma jamaa huyo kwa nyakati tofauti alishawahi kuripotiwa kubanjuka na mastaa wa Bongo Movies; Salma Jabu ‘Nisha’ na Skyner Ally ‘Skaina’ aliyezaa naye mtoto mmoja.


Loading...

Toa comment