The House of Favourite Newspapers

Nay wa Mitego Kimeumana Huko

0

TAYARI kimeumana huko! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya video ya Wimbo wa Acha Niongee wa Nay wa Mitego kufutwa kwenye Mtandao wa YouTube siku moja baada ya kuachiwa.

 

Kwa mujibu wa maelezo ya Mtandao wa YouTube, video hiyo imefutwa kutokana na madai ya hatimiliki ambayo yamepelekwa huko YouTube na mtu waliyemtaja kwa jina la Rashidi Said Madega.

 

Uamuzi huo wa YouTube unakuja saa kadhaa baada ya msanii Bright kudai kuwa Nay ameiba mdundo wa ngoma hiyo; ambayo walitakiwa kufanya pamoja, lakini baadaye Nay alibadilisha uamuzi na alitaka kufanya ngoma hiyo na Roma badala ya Bright.

 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Bright ameandika; “Wewe ndiye tajiri unayepokonya kidogo cha maskini kuweka mifukoni mwako Mungu utalipa yote uliyoyafanya kwenye muziki wangu nadili na wewe.

 

Huyu ni mwizi wa beat yangu ambayo nimeipiga mimi na nilimcheki nifanye naye wimbo (collaboration) akaleta tamaa huo wimbo wangu na beat yangu.”

Hadi sasa, Nay hajazungumzia chochote kuhusiana na sakata hilo.

Leave A Reply