The House of Favourite Newspapers

Morrison Alamba Milion 2

0

Kiungo mshambuliaji wa Simba Bernard Morrison, ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Novemba wa Simba.

 

Morrison amekabidhiwa kitita cha Sh 2,000,000 kama sehemu ya zawadi kutoka kwa wadhamini wa Klabu hiyo Emirate Aluminium ACP.

 

Morrison ameshinda tuzo hiyo kutokana na kuwa na kiwango bora katika mwezi huo akichangia kupatikana kwa mabao manne akifunga mawili na kusaidie mengine mawili.

 

Baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo Morrison amewasifu wachezaji alioingia nao fainali ya kinyang’anyiro hicho kuwa kila mtu alistahili kushinda lakini mshindi siku zote ni mmoja hivyo amefurahi kushinda.

 

“Nawapongeza pia nilioingia nao fainali wote tulistahili kushinda lakini mimi nimeibuka kidedea, nimefurahi na hii inanifanya kuendelea kujituma kuisaidia timu,” amesema Morrison.

Leave A Reply