Kartra

NBC Yakabidhi Vifaa Vyamichezo kwa Jeshi la Wananchi

Mkuuwa Kitengo cha Mauzo Wateja Binafsi Benki ya NBC, Bw Abel Kaseko (Kulia) akimkabidhi vifaa vya michezo Mwenyekitiwa michezo Kanda ya Ngome, Kanali David Mziray ikiwa ni msaada wa benki hiyokwenda kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya mashindanoya michezo mbalimbali ya majeshi yanayotarajiwa kuanza Agosti 4 mwaka huujijini Dodoma. Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika leo jijini Dodoma.Wanaoshuhudia ni maofisa wa benki hiyo pamoja na maofisa wa Jeshi la Wananchi.

Dodoma: Julai 16, 2021: Wakati mashindano ya michezo mbalimbali ya majeshi yanatarajiwa kuanzaAgosti 4 mwaka huu jijini Dodoma, benki ya NBC limetoa msaada wa vifaa vyamichezo kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ili kusapoti jitihada za jeshi hilokatika sekta michezo.

Vifaahivyo zikiwamo viatu vya michezo, mipira, jezi pamoja na vifaa vingine vyamichezo mbalimbali vilikabidhiwa kwa Mwenyekiti wa michezo Kanda ya Ngome,Kanali David Mziray, na Meneja wa NBC tawi la Dodoma, Bi Happiness Kizigira.

Mkuuwa Kitengo cha Mauzo Wateja Binafsi Benki ya NBC, Bw Abel Kaseko (Kulia) na Mwenyekiti wa michezo Kanda ya Ngome, Kanali David Mziray wakikata utepe kuashiria mahusiano mema baina yataasisi hizo mbili.

Akizungumzabaada ya kukabidhiwa vifaa hivyo, Kanali Mziray alisema vitasaidia kuongezahamasa kwa wachezaji wa timu za JWTZ ambao wamepania kuchukua vikombembalimbali vya mashindano hayo.

Menejawa benki ya NBC tawi la Dodoma Bi Happiness Kizigira (Kulia) akimkabidhi vifaavya michezo kwa mmoja wa maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa ajili yamaandalizi ya mashindano ya michezo mbalimbali ya majeshi yanayotarajiwa kuanzaAgosti 4 mwaka huu jijini Dodoma.

“Kupatakwa vifaa hivi kutawasaidia wachezaji wetu kuongeza hamasa zaidi kwenyemashindano hayo ambayo timu zetu zimepania kunyakua makombe yote,” alisemaMziray.

Menejawa NBC tawi la Dodoma Bi Happiness Kizigira akizungumza baada ya kukabidhivifaa hivyo, alisema wametoa vifaa hivyo kutokana na kuwapo na Ushirikiano katiya benki hiyo na jeshi la wananchi.

Maofisawa benki ya NBC pamoja na maofisa wa Jeshi la Wananchi wakiwa kwenye picha yapamoja wakati wa hafla hiyo.

“Benkiya NBC tumekuwa na mahusiano mazuri ya muda mrefu na Jeshi la Wananchi na kwakuwa mwezi ujao wenzetu watakuwa na jambo lao hapa Dodoma ambalo kimsingitunawaombea mafanikio sana tumeona ni vema tuwaunge mkono ili mambo yaende vizuri zaidi,’’ alisema Kizigira.

 

Kizigiraalisema vifaa hivyo wamevitoa Makao Makuu ya Jeshi kwa lengo la kuwezakuwafikia wanamichezo wote wa jeshi hilo ambao watashiriki mashindano hayomwaka huu.


Toa comment