The House of Favourite Newspapers

NBC Yazindua Klabu Ya Biashara Masasi, Yatoa Mafunzo ya Biashara

0
Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Selemani Mzee (Wa Nne Kushoto), akipiga makofi wakati wa uzinduzi wa NBC Business Club kwa Wilaya ya Masasi. Wengine katika picha ni Meneja wa tawi la NBC Masasi,  Erick Mbeyale ( wa kwana kulia) na Meneja wa Bidhaa na Huduma za Kifedha NBC, Jonathan Wilson (wa pili kulia) pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo.

Meneja wa Bidhaa na Huduma za Kifedha wa NBC, Jonathan Wilson akizungumza na wafanyabiashara wa Wilaya ya Lindi wakati wa uzinduzi wa NBC Biashara Club kwa Wilaya ya Masasi. 

 


 

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeendelea na mpango wao wa  kuanzisha NBC Biashara Club katika wilaya mbali mbali ikiwemo Masasi kwa lengo la kuwakutanisha wafanyabiashara na kuwapa nafasi ya kujadiliana changamoto zao na kupeana fursa mbalimbali. NBC Biashara club inawawezesha wafanyabiashara kupanua wigo wa biashara zao wa njia ya Mikopo ya muda, Huduma za ziada za kibenki, Ufundi wa kigheni, POS, Benki ya mtandao, Akaunti za sasa, Dhamana za Benki, Wakala wa Benki na Bidhaa za Bima.

 

Klabu ya Biashara ya NBC hutumiwa kama sehemu ya utunzaji wa biashara na mkakati wa uaminifu wa wateja. Kusudi kuu ni utoaji wa huduma za msaada zisizo za kifedha kupitia mafunzo ya ustadi wa biashara na kuwajengea uwezo kwa wateja wa biashara wa NBC, kama sehemu ya safari yetu katika kuwaunga mkono.

 

Akiongea katika hafla ya NBC Business Club iliyofanyika katika Hotel ya Rock City Wilaya ya Masasi, Meneja wa bidhaa na huduma za kifedha NBC Makao makuu Dar es salaam, Bw. Jonathan Wilson Bitababaje alisema, wamezindua NBC Business Club zaidi ya maeneo kumi na moja na Mtwara ikiwa eneo la kumi na mbili ivyo wameandaa fomu maalumu ambazo wafanyabiashara watajisajili kua mwanachama wa klabu iyo na watapata faida mbali mbali ambazo zitawasaidia kuendesha biashara zao.

 

Faida alizotaja Bw Jonathan Bitababaje ni, Mafunzo ya kukuza na kuendeleza biashara zao, Namna ya kupata mitaji, Namna ya kujua soko, Kuwakutanisha na wanachama wa Biashara Club kutoka mikoa mbali mbali, Jinsi ya kuendesha biashara zao kwa faida, Punguzo la bei kwa bidhaa za NBC na Safari za nje ya nchi amabzo wamekua wakitoa toka mwaka 2017.

 

Aidha alisisitiza wafanyabiashara kutunza kumbukumbuka za ulipaji wa kodi kwani itawasaida kuendesha biashara zao kwa faida. Pia alisema Klabu iyo itawasaida kuwapa taarifa mbali mbali kuhusu fursa zilipo ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania pamoja na kuwapa elimu ya mafunzo stahiki kwa ajili ya kuendana na ukuaji wa teknolojia.

 

Jonathan alimalizia kwa kusema Serikali imekua mdau mkubwa wa benki iyo na ni mmliki wa benki iyo kwa asilimia 30, ivyo ni muhimu kufwata taratibu zilizowekwa na serikali kwa ajali ya wateja wao. ‘’ Serikali imeweka fursa mbali mbali kwa ajali ya wateja wetu na wateja wanazijua na kuzitumia kwa upana zaidi. Changamoto wanazozipata zitashughulikiwa na benki na serikali yetu.’’

 

Naye Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Bw Selemani Mzee aliunga mkono NBC kwa kusema Klabu iyo ya biashara iwe ni zoezi endelevu ili liweze kuleta tija katika mkoa wa Masasi.Aliongeza kusema kua, kadri watakavyo hudumia wafanyabiashara ndivyo watakavyozidi kuleta fedha kwenye benki.

 

Alisisitiza wafanyabiashara wa Masasi kua makini na kuchangamkia fursa zinazojitokeza ili waweza kujiendeleza ki Maisha. Pia walipendekeza utolewaji wa vyeti kwa wafanyabiashara ikiwa ni ishara wa kuwatia moyo.

 

Leave A Reply