The House of Favourite Newspapers

Ndege Iliyobeba Maofisa wa Umoja wa Ulaya (EU) Yawaka Moto, Yaua 5

malta1

Malta, Luqa: Ndege iliyokuwa imebeba Maofisa wa Umoja wa Ulaya (EU) yadondoka na kuwaka moto muda mchache baada ya kupaa katika Uwanja wa Ndege wa Malta huko Luqa majira ya saa 7.20 asubuhi leo Jumatatu.

Katika tukio hilo, watu wote watano waliokuwemo kwenye ndege hiyo wameripotiwa kufariki dunia.

Bado harakati za uokoaji zinaendelea, waokoaji wamesema uwezekano wa kukuta watu wakiwa hai ni mdogo sana.

Hakuna mtu yeyote aliyepona ndani ya ndege hiyo inayoelezwa kuwa ilikuwa ikitokea Misrata nchini Libya.

Waliofariki wanadhaniwa kuwa ni raia wa Ufaransa huku taarifa zikishindwa kueleza kama walikuwa ni maofisa wa usalama au raia wa kawaida.

Taarifa zinaeleza kuwa ndege hiyo ilikuwa ni ya Shirika la Frontex huku msemaji wa shirika hilo akikanusha kuwa ndege hiyo siyo ya shirika lao.

Comments are closed.