The House of Favourite Newspapers

Helkopta ya Urusi Yatunguliwa na Kuua 5 Syria

0

1

7

3

8

Helkopta ya kijeshi ya Urusi aina ya Mi-8 ikiteketea baada ya kutunguliwa.

2

9

5

6

Wananchi wakishuhudia mabaki ya helkopta hiyo ya kijeshi.

4

Helkopta iliyotungulia ni sawa na hii hapo juu.

WATU watano wamepoteza maisha baada ya helkopta ya kijeshi ya Urusi aina ya Mi-8 kutunguliwa na waasi kaskazini mwa Syria, maofisa wa Urusi wameeleza.

Kwa mjibu wa Wizara ya Ulinzi, helkopta hiyo aina ya Mi-8, ilikuwa na watu watano; wafanyakazi watatu na maofisa wawili wa kijeshi wakati ilipoangushwa katika Jimbo la Idlib.

Msemaji wa Ikulu ya Rais wa Urusi, Kremlin, amesema kuwa watu hao wote watano wamefariki dunia.
Helkopta hiyo ilikuwa ikirudi baada ya kupeleka msaada wa kibinadamu huko Aleppo.

Kwa mujibu wa kitengo cha habari cha Interfax cha Urusi, kimemnukuu ofisa mmoja akisema haijulikani ni kundi gani lililoiangusha helkopta hiyo.

Leave A Reply