The House of Favourite Newspapers

Ndoa ya Maya yamzulia balaa Johari

0

DAR Mwigizaji Mayasa Mrisho ‘Maya’ amefunga ndoa, lakini kwa upande mwingine, ndoa hiyo imemzulia balaa mwigizaji mwenzake wa filamu za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ baada ya kupewa maneno makali. 

 

Ishu ilikuwa hivi, mwigizaji Irene Uwoya aliyekuwa mmoja wa waalikwa wa sherehe ya harusi iliyofanyika katika Ukumbi wa Dunken House uliopo Mikocheni jijini Dar, alimvaa Johari kwa kumuambia watu wamemchoka kusubiri kwa muda mrefu bila kuona hata kuna mwanaume anajitokeza kumuoa.

Uwoya alimwambia Johari kuwa, tangu wamefahamiana miaka mingi iliyopita, wasanii wahenga waliokuwa kwenye Kundi la Kaole Sanaa, wengi wao wameolewa, lakini yeye bado yupo tu. “Ninakuomba Johari, hii sasa ni aibu iliyopitiliza, umeozesha watu wengi hadi sasa, hata Maya amekupita, sijui wewe imekuwaje?

 

“Wewe ni rafiki yangu, kuna wakati ninakufikiria, sikupatii jibu kabisa,” alisema Uwoya huku Johari akimtazama tu na kuishia kuguna kuashiria ameishiwa pozi la kuzunguza. Kutokana na maneno hayo kumuingia vilivyo Johari,  alipoteza raha kwa muda, jambo lililomtoa kwenye ‘mudi’ kwa muda fulani, lakini baadaye alionekana kurejea kwenye uchangamfu wake wa kila siku.

Hata hivyo, baadhi ya waalikwa waliokuwemo ukumbini humo, walimsihi Johari asikate tamaa kwani kama ipoipo tu na itafika wakati na yeye ataolewa. “Utaolewa shoga yangu wala usijisikie vibaya, mambo ya ndoa haya wakati mwingine ni bahati tu,” alisikika mmoja wa waalikwa aliyeomba hifadhi ya jina.

Kwenye sherehe hiyo iliyohudhuriwa na mastaa kibao, Maya aliweka wazi kuwa hakutaka mumewe mtarajiwa ajulikane kabla hadi siku ya harusi yake. Alisema aliamua kufanya hivyo ili sherehe yake inoge maana wengine walikuwa hawaamini kama kweli anaolewa, hivyo wangefika ili tu kuhakikisha.

“Sikutaka mtu yeyote amjue mume wangu. Ndiyo maana kila mtu alikuwa na shauku ya kumuona na kumjua maana wengine walijua wamepigwa changa la macho,” alisema Maya akimaanisha kuna watu walidhani wanatapeliwa pesa zao za michango ya harusi.

 

Sherehe hiyo ya Maya ilihudhuriwa na mastaa mbalimbali ambao walinogesha mambo, lakini bado aliweka ngumu kumtaja jina mwanaume huyo pamoja na kwamba IJUMAA WIKIENDA lilishapata picha zake. Gazeti hili linamtakia Maya kila la heri kwenye maisha yake mapya ya ndoa.

 

Stori: IMELDA MTEMA , Wikienda

Leave A Reply