The House of Favourite Newspapers

Ndoa ya Nicki Minaj, Meek Mill yazua mjadala mitandaoni

0

Meek-Mill-Nicki-MinajNew York, Marekani

IKIWA zimepita siku chache baada ya rappa machachari kutoka Marekani Meek Mill amvalishe pete ya dhahabu mpenzi wake Nick Minaj kwenye sherehe ya siku yake ya kuzaliwa hivi karibuni wapendanao hao  wameibua ‘headline’ kwenye Mtandao wa Kijamii wa Twitter baada ya Nick kuwauliza maswali mashabiki wake juu ya mahali pa kufanyia harusi hiyo akilenga ufukweni au kanisani.

Baada ya Nick, 33, kupost maswali hayo ndani ya muda mchache zaidi ya mashabiki wake 20,000 walitoa maoni yao huku kati yao 11, 600 walipendekeza ndoa ya wawili hao kufanyikia beach.

Hata hivyo Nick alionekana kuchukua maoni ya mashabiki wake baada ya kuwajibu kuwa atayafanyia kazi kwa ‘kudiscuss’ na Meek jambo linaloonyesha kuwa ndoa ya waoendanao hao inanukia.

Leave A Reply