The House of Favourite Newspapers

Ndugu wa Chama Kuwavaa Simba Taifa

UONGOZI wa Simba, umeweka wazi kuwa utacheza na Power Dynamos ya Zambia katika tamasha la Simba Day. Simba imepanga kucheza na timu hiyo kutoka nchini Zambia anapotokea kiungo wake, Clatous Chama katika mchezo utakaopigwa Agosti 6, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

 

Taarifa iliyotolewa na Simba imeweka wazi kuwa wiki ya Simba itaanza Agosti Mosi, mwaka huu kabla ya siku ya kilele ambapo watacheza na mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu ya Zambia na Kombe la Washindi Afrika.

 

Simba ambayo imeweka kambi nchini Afrika Kusini, mchezo huo wa kimataifa utakuwa ni wa tano kabla ya kuwafuata UD do Songo ya Msumbiji katika mchezo wa kwanza wa hatua ya awali katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Tayari Simba imeshacheza na Orbret Tvet, kabla ya kesho Alhamisi kuwavaa Platinum Stars kisha Julai 27, kucheza na Township Rollers kabla ya kumalizana na Orlando Pirates Julai 30, mwaka huu.

Ibrahim Mussa, Dar es Salaam

Comments are closed.