NEC yasitisha Ajira Iliyozitangaza, Yaomba Radhi

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk Athuma Kihamia

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesitisha ajira za muda iliyozitangaza kwa ajili ya shughuli ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.

 

Mei 30, 2019 NEC ilitoa tangazo la ajira hizo na kuwataka Watanzania wenye elimu ya kidato cha nne na umri wa kati ya miaka 18 na 45 kuomba nafasi hizo kupitia tovuti yao.

 

Sifa nyingine zilizotakiwa ni uwezo wa kutumia kompyuta na awe hajawahi kutiwa hatiani kwa kosa la jinai pia awe na uwezo wa kufanya kazi katika mazingira yenye usimamizi mdogo.

 

Hata hivyo, taarifa ya Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk Athuma Kihamia aliyoitoa leo Alhamisi Juni 6, 2019 imesema mchakato wa ajira hizo umesitishwa hadi pale itakapotangazwa tena.

 

“Tume inapenda kutoa shukran zake kwa wale wote walioleta maombi yao ya kazi na inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza,” amesema Dk Kihamia


Loading...

Toa comment