The House of Favourite Newspapers

Nelly Muosha Magari wa Posta-34

0

Mpenzi msomaji, wiki iliyopita niliishia pale Nelly alipomfahamisha mama yake kwamba alikuwa akifanya kazi ya kuosha magari Posta, mama huyo akashindwa kujizuia kucheka na kuamua kumwuliza. Alimwuliza nini? Songa mbele…

“Yaani wewe Nelly ninayekufahamu umeamua kuosha magari tena Posta?”
“Ndiyo maana yake, mbona nilikuwa nafanya kazi ya ujenzi bila matatizo, tena mama naona kazi ya kuosha magari inalipa zaidi kuliko ya ujenzi,” Nelly alimwambia mama yake ambaye hakujua nyuma ya kazi hiyo kulikuwa na nini.

Mama huyo alicheka na kumwambia alimfurahisha kwa kuamua kufanya kazi yoyote ilimradi apate fedha, kwa furaha aliyokuwanayo akaenda kumwambia mumewe.
“Mimi nilikuambia kitafika kipindi huo usharobaro wake utaisha, umeniamini mama Nelly?” baba Nelly alimwambia mkewe, wakacheka.

Wakati mke na mume wanazungumza chumbani, Nelly alipomaliza kujiandaa ile anatoka kwenye korido akamuona baba yake akamwamkia.

“Vipi nasikia kule kwa fundi Yassin hauendi umeanza kazi ya kuosha magari Posta?” baba yake alimwuliza.
“Ni kweli baba, si unajua maisha ya leo hayahitaji kuchagua kazi!” Nelly alimwambia mzazi wake.
Baba yake alifurahi na kumweleza kikubwa afanye kazi hiyo kwa uaminifu na kuwaheshimu watu wote atafanikiwa kwani wengine wanaweza kumpa msaada mkubwa.

Nelly alipomaliza kuzungumza na baba yake alielekea nyumbani kwa akina Ipyana, akamkuta msichana wao wa kazi aitwaye Kisa akifanya usafi, alipomuuliza kama Ipyana alikuwepo akamwambia alikuwepo.
Kijana huyo mpenda mademu wazuri alivutiwa sana na kifua cha Kisa kilichopambwa na viembe bolibo vya kuchoma akaamua kumuweka kiporo, akaelekea geto kwa rafiki yake.

Marafiki hao walipopeana hi hawakuona sababu ya kuchelewa wakaenda kupanda gari na kuelekea Posta, njiani Ipyana kila alipomtupia macho Nelly akawa anatabasamu tu!
“Vipi naona unanitazama na kuachia tabasamu kulikoni?” Nelly alimwuliza Ipyana.
Rafiki yake huyo alimwambia alifurahishwa na mambo yake hasa jinsi alivyomuaga jana kwamba anakwenda kumuona mshkaji wake kumbe alikuwa na miadi na totoz.

“Huo ndiyo uanaume, ukiwa na fedha mfukoni lazima utafute kiburudisho tena jana nilikula bata ndefu na dogo aliondoka akiwa kachoka balaa kwa swaga nilizompa,” Nelly alijisifia ujinga.

Ipyana aliishia kucheka na kumwambia lakini pale wizarani ndiyo itakuwa mwisho wake asipokuwa makini kwani palikuwa na wanawake wazuri na wenye fedha zao wapenda viserengeti boy.
“Umakini gani kaka au unazungumzia ngoma nini?” Ipyana alimwuliza.
“Ndo maana yake,” Ipyana alimjibu.

Alipoambiwa hivyo Nelly alicheka na kumwambia asiwe na wasiwasi kilichozaliwa lazima siku moja kife, iwe kwa maradhi au kwa sababu zingine hivyo hawezi kumuacha mwanamke yeyote atakayejipendekeza kwake eti kwa kuogopa kufa.
Kufuatia stori kunoga wakajikuta wamefika Posta, waliteremka na kwenda eneo lao la kazi, kama ilivyokuwa siku ya kwanza wafanyakazi kibao wa wizara hiyo wakiwemo mabosi waliwachangamkia vijana hao.

Siku hiyo mishale ya saa mbili kasoro alifika dada Fatu aliyemchangamkia sana Nelly na kumfahamisha Ipyana kwamba alikuja na gari lake lingine alilotaka lioshwe na Nelly kufuatia jana yake kumuoshea vizuri gari aliloliacha nyumbani.

“Nelly nafikiri umemsikia dada Fatu kakupa tenda hiyo, kazi kwako,” Ipyana alimwambia Nelly aliyeishia kucheka.
Kabla Nelly  hajasema chochote Fatu akachomoa noti ya shilingi elfu tano akawaambia ya chai na kumuomba Nelly jioni watakapotoka kazini aende naye nyumbani kwake akamsaidie kazi f’lani.
“Kazi gani dada Fatu?” Ipyana alimwuliza dada huyo.

“Na wewe Ipyana bwana,  akija kuifanya atakwambia ninyi si marafiki?” Fatu alimwambia.

Je ni kazi gani ambayo dada Fatu anataka Nelly akaifanye? Usikose wiki ijayo. Maoni nicheki kwa namba hiyo hapo juu.

Leave A Reply