The House of Favourite Newspapers

Netflix Wapiga Chini Ofa Ya Apple

 

KAMPUNI maarufu ya filamu ya Netflix  ya Marekani imepiga chini dili walilolipata kutoka kwa washindani wao, kampuni ya Apple, ambao wanategemea kuzindua huduma yao ya mtandao wa video.

 

Mkurugenzi mkuu wa Netflix alisema Jumatatu iliyopita: “Tunapendelea wateja wetu kuangalia maudhui yetu ndani ya mitandao yetu, tumeamua kutokuunganisha na huduma zao”.

 

 

Kampuni ya Apple inategemea kuzindua huduma yao mpya ya televisheni na huduma ya kutazama video katika tamasha lao litakalofanyika Machi  25 mwaka huu ambalo limekusudiwa kuwa na ushindani na kampuni ya Netflix na kampuni nyingine.

 

Walipoulizwa juu ya ushindani na kampuni nyingine walisema kwamba changamoto kubwa kwa Netflix si kupata faid bali ni kujifunza maarifa zaidi.

 

Watakwenda kufanya tamasha kubwa sana, nitakuwa na wivu juu ya hilo kwa sababu watakuja na jambo kubwa sana, tutahitaji japo kuzichukua, ila tutakuwa na kampuni bora kama tutapata washindani wakubwa kama hao” alimaliza Reed Hastings mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Netflix.

Comments are closed.