The House of Favourite Newspapers

Zifahamu faida, madhara ya kula ‘kitimoto’

 

PAMOJA na mivutano ya kidini kuhusu utumiaji wa nyama ya nguruwe (kitimoto), suala hili linaelezewa kitaalam kwa mujibu wa tiba za  MEDICINE (Science)!!

 

Nguruwe ni mnyama anayeliwa na asilimia 38 ya watu wote duniani ambapo walaji wake wakubwa ni nchi Magharibi na Kusini mwa Asia, Ulaya, kusini mwa Jangwa la Sahara, America ya Kaskazini na Kusini, na eneo la  Oceania.

 

 

Faida za nyama ya nguruwe kitaalam: 

1. Ina vitamin muhimu katika mwili wa binadamu; ambazo ni B1, B6 and B12

2. Ina madini ya chuma ambayo husaidia kuimarisha mifupa.

3. Inaimarisha ngozi yako na kuifanya iwe laini.

4. Ina madini ya magnesium kwa wingi yenye faida kwa binadamu.

5. Ina protein ya kutosha inayosaidia ulinzi wa mwili.

6. Ina mafuta yanayotoa nguvu mwilini.

 

 

Madhara ya kula nyama ya nguruwe:

Licha ya faida zilizotajwa hapo juu, pia kuna hasara ya kutumia nyama hii ambayo ina sumu ya carcinogen inayosababisha kansa.

 

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani ( WHO) na The International Agency for Research on Cancer!! utafiti  unaonyesha kuwa ukila nyama hiyo kila siku gramu 50  uwezekano kupata kansa unaongezeka kwa asilimia 18.

Pia inasababisha homa iitwayo Swine Flu kwa binadamu ambayo inatokana na virusi vinavyosababisha mafua kwa binaadamu. Kwa mujibu wa utafiti uliofanyiwa na Centers for Disease Control and Prevention inaonyesha virusi vya Influenza  H1N1 na H3N2 vinavyotokana na kiti moto, kusababisha maradhi ya mlipuko kwa nchi za bara la Amerika.

 

 

Vilevile, nyama ya nguruwe ina minyoo wajulikanao kwa jina la trichinella worm  ambao ni vigumu kufa kwa joto hata la Centigrade 100.

Utafiti uliofanyiwa na WHO mwaka 1988, ulionyesha kitimoto  iliyopiwa kwa joto la C. 104,  asilimia  52.37  ya trichinella worm huwa wanabaki hai.

 

Wadudu hao wakiingia  mwilini mwa binadamu husababisha ugonjwa ujulikanao kwa jina la trichinosis; ambao huwa na dalili zifuatazo:

(i) Homa kali
(ii) Kichwa kuuma
(iii) Kukosa nguvu
(iv) Maumivu ya nyama za mwili
(v) Macho kuwa rangi ya pink (conjunctivitis)
(vi) Kuvimba uso na kope
(vii) Kudhurika  na mwanga
(viii) Kitimoto ina virus aina ya Hepatitis E virus (HEV) ambaye husababisha homa ya ini aina E

Wadudu wengine katika kitimoto ni:
(i)  Virusi vya Nipah virus
(ii) Menangle virus
(iii) Viruses katika  kundi la Paramyxoviridae
Wote hao huwa wana madhara kwa binadamu

 

Nyama ya nguruwe husababisha maradhi yanayokianza na madawa yenye kupambana na vimeleo vya magonjwa, yaani ‘Antibiotics’ na kwa mujibu wa WHO nyama ya hiyo pia ina minyoo aina ya Taenia solium.

Minyoo hii hutokana kutopikwa vizuri nyama hiyo.  Minyoo hii ikiingia mwili wa binadamu husababisha matatizo ya mfumo wa fahamu (central nervous system) iitwayo neurocysticercosis, na kusabisha kifafa.

Asimilia 3 ya wagonjwa wenye kifafa huwa ni wale ambao hushambuliwa na minyoo hii ipatikanayo kwenye nguruwe.

Watu milioni 50 duniani wanaopata kifafa  huwa ni walaji wazuri wa nguruwe.

Comments are closed.