The House of Favourite Newspapers

Ngoma amtumia Kaseke kumtengenezea mabao

0

DONALD-NGOMA3.jpgMshambuliaji tegemeo wa Yanga, Donald Ngoma.

Wilbert Molandi, Dar es Salaam
KATIKA kuhakikisha anaendelea na kasi yake ya kupachika mabao, mshambuliaji tegemeo wa Yanga, Donald Ngoma amekaa kikao kwa dakika tano na nyota, Deus Kaseke ili kujadili jambo.
Ngoma raia wa Zimbabwe mwenye mabao nane hadi hivi sasa, alifanya kikao na kiungo huyo kwenye mazoezi ya mwisho yaliyofanyika Uwanja wa Boko Beach Veteran jijini Dar hivi karibuni.
Straika huyo alikaa na kikao na kiungo huyo mara baada ya Kocha Hans van Der Pluijm kuwataka wachezaji wote kwenda nje kunywa maji.
Wakati wachezaji wengine wanakwenda nje kwa ajili ya kunywa maji na kupumzika nyota hao walibaki uwanjani na kufanya kikao chao binafsi.

Ngoma-3.jpg
Katika maongezi yao wachezaji hao, Ngoma alionekana akimpa mbinu na maelekezo ya jinsi ya kumpa pasi kwa njia tofauti ikiwemo kumpigia krosi safi.

Wakati Kaseke anapewa maelekezo hayo, mwenyewe alionekana akitingisha kichwa akimaanisha kuelewa na kutekeleza kile anachokihitaji na baadaye kuendelea na program ya kocha wao.

Mara baada ya mazoezi hayo kumalizika, Kaseke aliliambia Championi Jumamosi kuwa, kikubwa Ngoma alikuwa anampa maelekezo ya jinsi ya kucheza pamoja kwa kupasiana wakati akiwa na mpira wakishambulia goli la timu pinzani.
“Timu siku zote inatengezwa kwa ushirikiano na kikubwa kucheza pamoja na kuzoeana, Ngoma alikuwa anajaribu kunipa mbinu mbalimbali za jinsi ya kucheza pamoja wakati nikiwa na mpira tukishambulia goli la timu pinzani,” alisema Kaseke.

Leave A Reply