The House of Favourite Newspapers

Nguli wa Madawa ya Kulevya Duniani Akamatwa Dubai

0

MAOFISA mjini Dubai wamethibitisha kumkamata mmoja wa walanguzi wakubwa kabisa wa dawa za kulevya wanaotafutwa ulimwenguni pamoja na mshirika wake wa karibu, baada ya miaka mingi ya kuwa mafichoni.

 

Raffaele Imperiale, raia wa Italia, anayechukuliwa kuwa mmoja wa wahalifu hatari zaidi nchini Italia, alikuwa mlanguzi mkuu kwenye mtandao wa uhalifu wa kupangwa mjini Napoli. Katika mwaka wa 2016 alisadikika kukimbilia Dubai, ambayo ni Emirati ya Ghuba.

 

Taarifa ya polisi ya Dubai imesema Imperiale amekamatwa pamoja na mshirika wake Raffaele Mauriello, ambaye alihusika na kupanga na kufanya mauaji kwa kutumia silaha haramu. Polisi imesema mshukiwa huyo amekuwa akiishi kwa utambulisho bandia akitumia jina la Antonio Rocco.

 

Polisi mjini Napoli imesema Imperiale alikamatwa Agosti 4 mjini Dubai kwa ushirikiano na polisi wa  kimataifa ya Ulaya.

Leave A Reply