The House of Favourite Newspapers

Ni Kweli Paula Anasomea Udaktari? Wanafunzi Wanaosomea Fani ya Udaktari Wafunguka

0
Mrembo maarufu kwenye mitandao ya kijamii (sosholaiti), Paula Kajala.

 

PAULA Kajala au Pau; ni mrembo maarufu kwenye mitandao ya kijamii (sosholaiti) ambaye baadhi ya wanafunzi wanaosomea fani ya udaktari katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili wameonesha shaka kwamba ni kweli naye anasomea udaktari?

 

Mwaka jana, Paula alikwenda masomoni nchini Uturuki ambapo alieleza kwamba anasomea masomo ya udaktari, lakini mwanzoni mwa mwaka huu alirejea nchini kwa madai kwamba yupo likizo hadi mwezi Agosti ndipo atarejea masomoni.

 

Baadhi yao waliopiga stori na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA wamehoji kwamba, inawezekanaje mtu akawa anasomea fani kubwa kama hiyo, halafu akapewa likizo ndefu kuliko muda wa kusoma?

 

Hata hivyo, wanafunzi hao walifafanua hoja kuwa, inakuwaje Paula akaenda kusoma udaktari wakati ameishia kidato cha nne na kufeli ambapo wenyewe wanasema inawezekana kwa mtu aliyesomea masomo ya sayansi; yaani Biology, Chemistry na Physics ambapo anaweza kutumia cheti cha kidato cha nne kuanzia kwenye ngazi ya cheti kisha diploma na baadaye shahada.

STORI; IJUMAA WIKIENDA, DAR

MO AMWAGA MAMILIONI SIMBA, VYUMA VYAANZA KUSHUSHWA, HERSI AFICHUA USAJILI YANGA | KROSI …

Leave A Reply