The House of Favourite Newspapers

Ni vita ya Kaseja na Makambo Taifa

KIPA mwenye heshima kubwa nchini ambaye kwa sasa anaichezea KMC, Juma Kaseja, amesema hawamuhofii Heritier Makambo bali wanaihofia Yanga. Kaseja ametoa kauli hiyo ambapo leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar timu hizo zitapambana ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.

 

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa uwanjani hapo, Yanga iliifunga KMC bao 1-0  kupitia kwa mpira wa faulo uliopigwa na Feisal Salum ‘Fei Toto’ dakika ya 89 ambapo golini alikaa Kaseja.

 

Spoti Xtra lilipomuuliza Kaseja hahofii kukutana na Makambo wa Yanga mwenye mabao 12, alisema: “Sisi KMC hatumuhofii mchezaji bali tunaihofia Yanga nzima kwa sababu ni timu kongwe na kubwa kushinda yetu.

 

“Tumejipanga kukabiliana nao na tunaamini kwamba atakayekuwa na bahati ndiye ataibuka na ushindi na si vinginevyo,” alisema Kaseja ambaye aliwahi kucheza Yanga na Simba na kuvuna mamilioni

Comments are closed.