The House of Favourite Newspapers

NI VYAKULA GANI VINAVYOONGEZA NGUVU ZA KIUME?

POLE na kazi Anko, mimi ni mwanaume mwenye umri wa miaka 37. Tatizo linalonisumbua, ni kwamba katika siku za hivi karibuni nimekuwa nikisumbuliwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Sitaki kutumia madawa makali ya hospitalini, nimesikia kwamba yana madhara. Je, naweza kujitibu tatizo hili kwa vyakula vya aina gani?

Msomaji, Dar es Salaam.

 

Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume linawasumbua wanaume wengi hasa maeneo ya mijini na siku hizi kumeibuka wimbi la matapeli wanaojinufaisha kupitia tatizo hilo kwa kutangaza kwamba wanazo dawa za kurudisha nguvu za kiume. Japokuwa wapo wanaosaidia kweli, lakini wengi ni waongo na wanachangia kulifanya tatizo kuzidi kuwa kubwa.

 

Uamuzi wa kutumia vyakula kujitibu tatizo hili ni wa busara zaidi na wasichokijua wengi ni kwamba unaweza kabisa kumaliza tatizo hili kwa kula vyakula vyenye uwezo wa kumuongezea mwanaume nguvu awapo kwenye tendo.

 

Vyakula hivyo ni pamoja na karanga, vitunguu swaumu, ndizi mbivu, pweza na chaza, parachichi, pilipili, kunazi (blueberries), tikiti maji, mihogo, nazi, mbegu za maboga, mboga za majani, komamanga, asali, mvinyo mwekundu na tangawizi.

 

Pia hakikisha unafanya mazoezi angalau mara tatu kwa wiki kwa muda usiopungua nusu saa, epuka vyakula vya mafuta kama chipsi na zaidi pendelea vyakula vya nafaka isiyokobolewa kama ugali wa dona na kadhalika. Pia kunywa maji ya kutosha kila siku.

Na Anko Hash, 0719401968

EXCLUSIVE: Mama mkwe wa ‘MUNA’ kapasua Jipu! “Kweli ana Mtoto”

Comments are closed.