The House of Favourite Newspapers

Nicki Minaj Afunga Ndoa Kimyakimya!

STAA wa muziki wa hip-hop nchini Marekani, Nicki Minaj, amewashtua mashabiki zake baada ya kubadilisha jina la kwenye akaunti yake ya Twitter na kujiita Mrs Petty.

 

Kitendo cha kubadili jina kimeacha maswali mengi kwa mashabiki huku wakiamini tayari rapa huyo amefunga ndoa kimyakimya na mpenzi wake, Kenneth Petty.

 

Wiki mbili zilizopita wawili hao walifanikiwa kupata kibali cha kufunga ndoa ambapo kibali hicho hudumu kwa siku 90 tangu kukipata, hivyo wiki iliopita Nicki aliweka wazi kuwa watafunga ndoa ndani ya siku za kibali hicho.

 

Mashabiki wanaamini tayari wawili hao wamefunga ndoa japokuwa kati yao hakuna aliyeweka wazi kama kweli wamefanikisha jambo hilo.

Comments are closed.